'Maumbile yangu ni ya kiume lakini jinsia yangu ni ya kike'
Sharon alizaliwa kama huntha mwenye jinsia mbili -ya kike na ya kiume."Wakati nimeanza kubaleghe nilikuwa na mahangaiko mengi mno , kwani mwili wangu ulianza kubadilika ukiegemea upande wa kiume zaidi , ila kiashiria cha jinsia yangu kilikuwa kimesalia cha kike baada ya upasuaji. Sharon @sharonngeru ndiye mgeni wetu wa leo katika Waridi wa BBC jukwaa la wanawake na Anne Ngugi.Je anaishi vipi?Je anamwenza?Je nini husababisha hali hii ?•••#intersex #waridiwabbc #wanawake #mama #huntha #bbcswahili